Anti Suzy: Haya ndiyo machungu ya ushoga


Haya ndiyo makazi ya Anti Suzy pembezoni mwa mto Msimbazi jijini Dar es Salaam. Picha na Florence Majani 

Vitendo vya Ibrahim Mohamed Anti Suzy havikuwapendeza watu wengi hasa wanaume. Alipingwa mitaani, barabarani na maisha yake yakawa ya kujificha mithili ya panya.

“Niliwahi kupanga nyumba karibu na msikiti, majirani na viongozi wa msikiti wakaamua kunifukuza wakasema nitawafundisha watoto wao tabia mbaya. Wakanirudishia kodi yangu nikaenda kupanga chumba kingine”anasema

Si hivyo tu, bali anazomewa barabarani, kutukanwa, wakati mwingine watu kukataa kumpa mikono au hata kumsaidia anapougua.

Anti Suzy anasema, moja ya tabu zake kuu ni kuingiliwa na wanaume na kubakwa mara kwa mara jambo ambalo linamkosesha raha hasa ukizingatia nyumba yake ni chakavu.

“Juzi waliniingilia wanaume wanne, walifika usiku saa tisa, wakasukuma mlango kwa nguvu, wakanibaka wote,” anasema.
Kijana huyu anasema pamoja na kuwa na tabia za ushoga, mwendo wake, sauti na jinsi alivyo havifichi kubaini kuwa ni mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Anasema anapovaa mavazi ya kiume, ndipo watu humshangaa kwani anakuwa na sura ya kike, mwendo wa kike, sauti ya kike kasoro mavazi tu.

“Lakini nikivaa khanga au sketi ndefu, hakuna mtu anayejua kuwa mimi ni mwanamume na nimeshawahi kupata mwanaume alidhani mimi ni mwanamke alipofika chumbani alitimua mbio” anasema.

Mwaka 2010 Anti Suzy alikwenda kupima virusi Vya Ukimwi na hapo alipewa majibu yaliyomshtua ambayo hata hivyo hakuyaamini majibu hayo.

Anasema hakuweza kuamini majibu ya kuwa ana VVU kwa sababu alikuwa na afya njema, alikuwa haumwi chochote kile.

“Nilipima hospitali zaidi ya tatu, Bugando, Muhimbili na Kilimahewa na majibu yalikuwa yaleyale kuwa ni nimeathirika” anasema

Anti Suzy hata hivyo hakuacha tabia hiyo, aliendelea akiamini kuwa hiyo ndiyo njia ya kujipatia kipato chake cha kila siku, hadi mwaka jana hali yake ilipokuwa mbaya zaidi.
Previous
Next Post »