WHO yatoa tahadhari ya ugonjwa wa Nimonia Tanzania unaosababishwa na virusi vya Corona.

mw

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi.

 

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Nimonia unaosababishwa na kirusi cha “Novel Coronavirus”.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa tangu ugonjwa huo utokee mwishoni wa mwaka 2012 hadi tarehe 23 Mei 2013  idadi ya wagonjwa wapatao 44 na vifo 22 vimeripotiwa

Shirika la Afya Duniani limethibitisha ugonjwa huo kuwepo katika nchi za Mashariki ya Kati  yaani Jordan, Qatar, Saudi Arabi na Falme za Kiarabu (UAE).

Katika bara la Ulaya, ugonjwa huu umethibitishwa kutokea nchi za Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza.

Wakati katika bara la Afrika, ugonjwa huo umetokea Tunisia.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale wanaosafiri kuelekea maeneo tajwa yenye uthibitisho wa ugonjwa huo.

Previous
Next Post »