MWANAUME aliyegeuza jinsia yake, amelishtaki baraza la mitihani nchini, Kenya National Examination Council (KNEC), akitaka lishurutishwe kubadilisha vyeti vyake kuonyesha kwamba ni mwanamke.


 

BAADA YA KUJIBADILISHA

Paul Wasanga

 
 

Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) Paul Wasanga.


 
Bi Audrey Mbugua ambaye awali alifahamika kwa jina la Andrew Ithibu kabla ya kubadilisha jinsia yake, anataka cheti chake cha mtihani wa kidato cha nne (KCSE) kionyeshe kwamba ni mwanamke.
Aliambia mahakama kwamba aligunduliwa kuwa na dosari ya jinsia 2001, na amekuwa akikabiliana na shida nyingi kwa sababu anatambuliwa kama mwanaume katika vyeti vyake

“Nimejaribu kuomba KNEC mara nyingi ibadilishe jina langu katika cheti changu vya mtihani wa KCSE ili kionyeshe jinsia yangu halisi bila kufaulu,” Bi Audrey aliambia mahakama.

Alisema hatua ya KNEC kukataa kufanya mabadiliko hayo, imemsababishia mateso mengi kwa kubaguliwa na kunyimwa kazi. Mahakama ilimruhusu kuwasilisha ombi la kutaka baraza hilo liagizwe kutekeleza majukumu yake kwa kurekebisha jina lake liwe na mwanamke.

Siku 14

Anataka pia baraza hilo iagizwe kubadilisha alama inayoonyesha jinsia yake inayoonyesha ni mwanaume katika cheti hicho na badala yake ionyeshe kuwa ni mwanamke.

Mahakama ilipatia KNEC na Mkuu wa sheria muda wa siku 14 kujibu ombi la Bi Audrey.

Kesi itatajwa Mei 28 ili mahakama itoe maagizo zaidi.

Previous
Next Post »