BAADA YA KUJIBADILISHA
Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) Paul Wasanga.
|
Bi Audrey Mbugua ambaye awali alifahamika kwa
jina la Andrew Ithibu kabla ya kubadilisha jinsia yake, anataka cheti chake cha
mtihani wa kidato cha nne (KCSE) kionyeshe kwamba ni mwanamke.
Aliambia
mahakama kwamba aligunduliwa kuwa na dosari ya jinsia 2001, na amekuwa
akikabiliana na shida nyingi kwa sababu anatambuliwa kama mwanaume katika vyeti
vyake
“Nimejaribu kuomba KNEC
mara nyingi ibadilishe jina langu katika cheti changu vya mtihani wa KCSE ili
kionyeshe jinsia yangu halisi bila kufaulu,” Bi Audrey aliambia mahakama.
Alisema hatua ya KNEC
kukataa kufanya mabadiliko hayo, imemsababishia mateso mengi kwa kubaguliwa na
kunyimwa kazi. Mahakama ilimruhusu kuwasilisha ombi la kutaka baraza hilo
liagizwe kutekeleza majukumu yake kwa kurekebisha jina lake liwe na mwanamke.
Siku 14
Anataka pia baraza hilo
iagizwe kubadilisha alama inayoonyesha jinsia yake inayoonyesha ni mwanaume
katika cheti hicho na badala yake ionyeshe kuwa ni mwanamke.
Mahakama ilipatia KNEC na
Mkuu wa sheria muda wa siku 14 kujibu ombi la Bi Audrey.
Kesi itatajwa Mei 28 ili
mahakama itoe maagizo zaidi.
EmoticonEmoticon