INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.
Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia katika dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.
Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini.
Kikao cha dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi wetu kutoa maelekezo juu ya habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za jiji la Dar usafiri uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.
Haraka timu ya waandishi wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama.
Taarifa iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya kumuondoa denti huyo.
Wikiendi iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine amemwingiza yule denti chumbani kwake.
Timu A iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo la tukio na kuliweka chini ya uangalizi huku timu B ikielekea katika Kituo cha Polisi cha Wailesi na kuomba ushirikiano wao.
Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.
Waandishi wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa darasani.
Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.
“Ni kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa. Nyumbani kwetu ni Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni lakini Taliki aliniambia nije kwake.
“Naombeni mnisamehe jamani. Mama akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na ninaahidi mbele yenu kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba (Taliki),” alisema denti huyo.
Denti huyo alitoa namba ya simu ya mama yake mzazi ambapo alipigiwa na kufika eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto wake anavyoharibiwa wakati yeye akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea maisha.
Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.
UPUUZI WA TALIKI
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
“Ndugu zangu wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma (utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa anamtengenezea yule binti wa watu maisha?).”
Utetezi wake haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi Wailesi na kufunguliwa mashitaka katika Jalada nambaWS/RB/585/2013 – KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.
SOURCE :GPL
EmoticonEmoticon