Habiba
Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo
halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka
zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa
ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na
kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu
kiafya.
Tukio
hilo limetokea leo jijini mbeya katika mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo
majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika
nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake
.
Mtoto
huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa kuwa ni kati ya
miaka miwili au mitatu ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku
wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao
.
Akizungumzia
tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali
hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea
mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema
katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea taarifa kuhusiana na
suala hilo ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi
za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto
huyo.
Aidha
baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao
walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora
pamoja na huduma nyingine.
.
Mara
baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena
ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na
mke wake aitwaye Sekera Watsoni (40)
kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo
hilo.
Amesema
mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa
ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo
vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Kwa
upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio
waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza
mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto
wanawake.
Mmoja
wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto
ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka
hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto
huyo
Amesema
hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi
mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma
nyingine.
Amesema
anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao
wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya
kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa
katika kituo cha afya Inyala Kata ya Iyunga jijini
hapa.
Awali
inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu
sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo
ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa
sasa kama mama wa kambo.
Amesema
kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo
ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na
mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa
hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata
wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo
katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani
waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala
kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini
kinacho msumbua mtoto huyo
Picha
na Mbeya yetu
|
EmoticonEmoticon