LADY J DEE APIGWA STOP NA MAHAKAMA KUIONGELEA CLOUDS IN THE PUBLIC.


LADY JAYDEE AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kufuatia kufunguliwa kesi ya madai. Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo Mei 27, mwaka huu. Jaydee aliwasili mahakamani akiwa na mumewe Gadner G. Habash mida ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.
(Habari na Richard Bukos / GPL)
Jide na Mumewe wakiwasili mahakamani leo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee(Pichani) muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.

Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.

Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo
Previous
Next Post »