Kisa cha hivi karibuni cha Muasi nchini Syria kuula moyo wa
mwanajeshi aliyeuawa, kiliwashangaza wengi. Lakini tukio kama hili je ndilo la
kinyama zaidi kuliko matukio mengi yanayoshuhudiwa katika maeneo ya vita?
Tumezoea kusikia ripoti za makaburi ya halaiki, vyumba vya mateso, mauaji na
kukatwa katwa miili ya watu na hata kuwaangamiza watu katika kijiji kizima.Je ni nini kinachosababisha watu katika maeneo ya vita kufika kiwango hiki cha kula wengine?
Katika mahojiano na wapiganaji 2,500 wa zamani kutoka Uganda, Rwanda, Colombia na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
iligunduliwa kuwa vitendo vinavyofanyika katika maeneo hayo sio vichache ukilinganisha na kile kichotokea nchini Syria.
Kinyume na hilo, wakati maadili ya kijamii yanapoporomoka huku ghasia zikianza kutokea ishara ya vita, basi maadili yanayolinda binadamu kutokana na binadamu mwenzake nayo yanapotoka.
Kumuona mwathiriwa akiteseka humridhisha mshambuluaji na kuliona jambo hilo kama zawadi au tuzo kwake.
Kuna sababu mbili zinazomsababisha mtu kufanya kitendo mfano kama cha kumla mwenziwe.Na pili kuna hisia za kufurahisha, kuchangamsha na za raha tupu.
Hakuna anayejua sababu ya kutokea kitendo cha Syria na pili hakuna anayejua kilichomshinikiza yule muasi kufanya kitendo kile.
Kitendo hiki hakiwezi kukubalika, lakini kinaweza kueleweka ikizingatiwa matukio ya Syria (vita) ambavyo vimesababisha kutendwa kwa kitendo kile.
Kilitokana na hasira na hamu ya kulipiza kisasi. Binadamu wanaweza kufanya vitu ambavyo vinaonekana kwenda kinyume na ubinadamu.
Kunyongwa kwa Saddam Hussein au mauaji ya Bin Laden vinatukumbusha kuwa wakati mmoja binadamu wanaweza kukiuka maadili yao na kuua.Kanda inayoonyesha kitendo cha mauaji na picha ya damu ya mtu kwenye chumba chake huonekana kama tuzo baada ya uwindaji.
Kitendo hicho pia ni kumbusho la mapigano yanavyokithiri nchini Syria.
Mateso bila shaka huwa ni machungu kwa adui , ukataji wa viungo vya mwili mfano maskio , midomo na sehemu za siri ni vitendo vya kawaida katika vita na viko wazi katika maeneo mengi ya dunia.
Na kwa hivyo kitendo kilichoripotiwa Syria hakipaswi kuwashangaza wengi.
Takriban watoto milioni mbili wanakumbwa na jnaa, magonjwa na wameathirika kisaikolojia.
Kando na hilo,kuna makundi ya waasi ambayo huamua kula binadamu kama njia moja ya kuendeleza uasi wao.
Takriban asilimia 10 ya waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, walisema wamewahi kula binadamu na kwamba waliwahi kushuhudia wenzao wakila binadamu.
Wapiganaji wa Mai-Mai, nchini DRC , walikuwa na tabia ya kunywa damu ya adui wao na kula moyo au sehemu zao za siri wakiamini kuwa viungo hivyo viliwapa nguvu dhidi ya maadui wao. Hata hivyo hakuna ushahidi wowote wa kuwahi kutokea tabia ya watu kukulana Syria.
Hata hivyo kuna uwezekano kuwa kinachosahuhudiwa kwenye kanda hiyo ya video nchini Syria, ni kitendo ambacho kitakuwa kitu cha kawaida nchini Syria.
EmoticonEmoticon