katibu mkuu wa CCM Taifa Bw Kinana Kushoto) akiwa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe leo jimboni Ludewa
.....................................................................................................................................................
WAKATI kukiwa na tetesi za chini kwa chini ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kuwa chama hicho kimekuwa kikiwachukia wabunge wa CCM wanaokishambulika chama hicho bungeni akiwemo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mbunge wa jimbo la Mwibara Kang Lugola ambao wamekuwa wakiipinga serikali ,katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana amempongeza mbunge huyo na kumtaka aendelee na moto huo huo wa kuwapigania wananchi wake.
Hata hivyo kabla ya Kinana kumpa rungu mbele ya wsananchi mbunge Filikunjombe wananchi wa jimbo hilo walionyesha kumbana kiongozi huyo kwa kuhoji sababu ya wabunge wa CCM bungeni kufanya kazi ya kukipongeza chama chao huku wengi wao wakiwa kimya (mabubu) katika kuchangia na wale wanaochangia kama mbunge wao Filikunjombe wamekuwa waklichukiwa kuwa ni wapinzani ndani ya CCM .
Hivyo wananchi hao kumweleza katibu mkuu huyo aliyeongozana na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye kuwa wao wataendelea kumuunga mkono mbunge Filikunjombe kwa vipindi vingine tena tena vitatu vya miaka 15 tena hadi mbunge mwenyewe atakapoamua kuacha kugombea na iwapo watafanya mchezo basi wao watamfuata mbunge huyo kokote atakakokuwa.
" Mheshimiwa tunaomba leo chama kitueleze hivi kwanini wabunge wa CCM wamekuwa si msaada kwa wapiga kura wao muda wote wamekuwa kimya bungeni na wale wanaochangia wanachangia kupongeza chama .....sasa tunaomba kukueleza kuwa sisi tupo na mbunge wetu na hata wana CCM wanaojipitisha jimbo la Ludewa wakiamini sisi tutayumba uwaeleze kuwa CCM hatudanganyiki "
Akizungumza jana na wananchi wa wilaya ya Ludewa ambao walikusanyika kwa wingi katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kutaka kusikia kauli ya CCM juu ya uamuzi utakaochukuliwa kwa mbunge wao kutokana na kuwepo kwa kauli za chini kwa chini katika jimbo hilo kuwa ziara ya Kinana jimboni humo ni kutaka kumshughulikia mbunge huyo.
Akizungumza na wananchi hao Kinana alisema kuwa lazima wabunge wa CCM kuiga mfano wa Filikunjombe kwa kuwasemea wananchi waliowachagua na kuwa mbunge ambae amekuwa hawasemei wananchi wake bungeni hatoshi kuwa mbunge .
Hivyo kuwataka wananchi kuwa makini kwa kuwaangalia wabunge wao waliowachagua kuona kitu gani wanakifanya bungeni na kuwahukumu kulingana na kile wanachokifanya kama hawawasemei kuwa nao makini.
Hata hivyo Kinana aliwataka wananchi hao wanaounga mkono uamuzi wa kuendelea kumwongeza muda wa vipindi vitatu Filikunjombe kunyosha mikono juu na baada ya wananchi wote kunyosha mikono yao juu alisema pia kwa upande wake anaungana na wao na kuwa chama hakitafanya makosa kwa kuwasaliti kuwapa mtu mwingine katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 .
"Hata mimi katibu mkuu naungana na uamuzi wenu wa kumwongeza muda Filikunjombe na napenda kuwahakikishia kuwa CCM haitafanya makosa itaendelea kuwaachia Filikunjombe kama mlivyomchagua wenyewe labda ashindwe yeye "
Katika hatua nyingine Kinana alisema kuwa CCM hakitafanya makosa katika kuwateua wagombea wa nafasi mbali mbali na kuwa watakaoendelea kuteuliwa ni wale ambao wanafanya vizuri katika majimbo yao.
Aidha alikiri utendaji kazi wa mbunge Filikunjombe na kuwa ni m bunge wa mfano katika bunge na kuwa hata chama kinapendezwa na uchapakazi wake na kuwa mbali ya wananchi wa jimbo hilo kumwita ni jembe ila yeye kama Kinana anamfananisha mbunge huyo na katapila kwani amekuwa hamwogopi mtu katika utendaji kazi wake.
Pia alisema kuwa mbali ya Filikunjombe kufanya kazi vema ila bado ni kijana anayejituma na pia ni kwa kiasi ni mbabe katika kupigania wananchi wake .
Kuhusu shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na mbunge huyo Kinana alisema kuwa wao kama chama wanapendezwa na kazi za mbunge huyo na kuwa toka anaanza ziara ya siku mbili hakuna hata sehemu moja ambayo wanampinga mbunge huyo .
Awali akiwa katika kata ya Mlangali wananchi wa eneo hilo walimkana mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe na mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Pindi Chana kuwa hawamtambui mbali ya kuuwakilisha mkoa huo wa Njombe.
Wananchi hao walimkana mbunge huyo baada ya Kinana kuwauliza kama wanamtambua mbunge huyo.
Kwa upande wake Filikunjombe alisema mbali ya kuanza mradoi mkubwa wa lami katika wilaya hiyo ila bado kuna mradi wa maji wenye thamani ya Tsh bilioni 1.5 ambao utaondoa adha ya maji katika mji wa Ludewa.
Filikunjombe alisema kutokana na kuendelea kuutamani ubunge wake ataendelea kuwatumikia vema wananchi na kamwe siku zote hatarudi nyuma bungeni katika kuwapigania wananchi hao .
EmoticonEmoticon