HATIMAYE wasamaria wameanza kujitokeza katika kumsaidia mtoto Joshua Joseph ambaye alifungiwa ndani zaidi ya miaka miwili huku akikosa matunzo muhimu na kupelekea mtoto kupata ugonjwa wa utapia mlo.

 


Mwandishi wetu Joseph Mwaisango aliyembeba mtoto Joshua akiwa na ofisa maendeleo na ustawi wa jamii  Habiba Iblahimu
Mwandishi wetu Joseph Mwaisango akikabidhi msaada ya Magodoro, nguo na lishe kwa niaba ya familia ya Mama Masawe wa DSM ambayo iliguswa sana na hali aliyokuwanayo mtoto Joshua
Hakika mtoto Joshua sasa angalau siku mbili hizi hata kusimama na kutembea ameanza tunawashukuru wote mnaomsimamia mtoto huyu hapo ikuti Iyunga 
Mtoto Joshua akiangalia zawadi alizopatiwa
Mama mlezi wa Joshua akiwa haamini kabisa kwa msaada waliopatiwa kwa ajili ya Joshua
Yaani majirani wakibaki kuduwaa na kusema mungu awabariki kazi za mikono yao wote waliomchangia mtoto huyu na wasiishie hapo wawajali na watoto wengine Tanzania
 Balozi wa Mtaa wa Ikuti  Aron Mboya, aliwashukuru wasamaria hao na kwamba serikali ya kijiji itasimimia na kuhakikisha mtoto huyo anapata huduma zote za kiafya pamoja na kumsimamia mama mlezi kutumia misaada hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa mtoto huyo.
Daktari wa kituo cha Afya, Inyala kilichopo Kata ya Iyunga, Queen Mwakijambile, amesema baada ya vipimo kufanyika mtoto huyo amekutwa na tatizo la utapiamlo huku uzito wa mwili ukiwa haulingani na umri wake.
Mama mlezi wa Joshua akiwa kituo cha afya
Mtoto Joshua siku ya kwanza tulipomkuta alikuwa hivi


HATIMAYE wasamaria wameanza kujitokeza katika kumsaidia mtoto Joshua Joseph ambaye alifungiwa ndani zaidi ya miaka miwili huku akikosa matunzo muhimu na kupelekea mtoto kupata ugonjwa wa utapia mlo.
Moja ya Wasamaria hao Familia ya mama Masawe toka DSM wametoa magodoro mawili, nguo,mashuka,chakula pamoja na lishe ya mtoto.
Akipokea msaada huo jana, ofisa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamiii, Habiba Ibrahimu  alisema wasamaria hao wameonyesha  uzalendo na kuokoa maisha ya mtoto ambayo kwa asilimia kubwa yalikuwa hatarini.
Aidha, Daktari wa kituo cha Afya, Inyala kilichopo Kata ya Iyunga, Queen Mwakijambile, alisema baada ya vipimo kufanyika mtoto huyo amekutwa na tatizo la utapiamlo huku uzito wa mwili ukiwa haulingani na umri wake.
“Baada ya mtoto Joshua kufikishwa kwenye kituo hiki cha matibabu na kufanyiwa vipimo, tumebaini mtoto alikosa lishe pamoja na uzito wake kufikia kilo nane ukilinganisha na umri wake wa miaka miwili,”alisema
Alisema, uzito wa kilo nane ulipaswa kuwa na mtoto wa miezi sita au saba hivyo hatua aliyofikia alikuwa kwenye hatari ya kupoteza uhai wake.
Naye Balozi wa Mtaa wa Ikuti  Aron Mboya, aliwashukuru wasamaria hao na kwamba serikali ya kijiji itasimimia na kuhakikisha mtoto huyo anapata huduma zote za kiafya pamoja na kumsimamia mama mlezi kutumia misaada hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa mtoto huyo.

Picha na Mbeya yetu
Previous
Next Post »