Maiti ya Mwanamke Uliokotwa kwenye mashamba ya mkonge Mkoani morogoro hivi karibuni baada ya kujinyonga (picha na maktaba)
Mrembo mmoja mkazi wa Ihanzutwa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Neema Kisanga ( 35) ameuwawa kinyama na mpenzi wake baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na kupelekea fuvu la kichwa kupasuka kabla ya kunyongwa shingo.
Habari kutoka wilayani Mufindi ambazo zimethibitisha na viongozi wa serikali ya kijiji hicho zinadai kuwa tukio hilo May 11 mwaka huu katika kijiji hicho.
Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alikutwa na mauti hayo akiwa nyumbani kwake majira ya saa 6 usiku baada ya mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la Edward Mdegella kumvamia na kuanza kumpa kichapo hadi kusababisha kifo chake.
Mashuhuda hao walioteta na mtandao huu wa www.matukiodaima.com wanadai kuwa chanzo cha ugomvi huo uliosababisha kifo cha mrembo huyo ni wivu wa kimapenzi na baada ya kufanya mauwaji hayo mtuhumiwa alitoweka kusiko julikana
Source:Francis Godwin
EmoticonEmoticon