Naibu Katibu Mkuu wa baraza la Taifa la Mitihani, Dk. Charles E. Msonde.
Jumla ya watahiniwa 52, 513 waliandikishwa kufanya mtihani wa kidato cha sita 2013 wakiwemo wasichana 16,934 sawa na asilimia 32.25 na wavulana 35,579 sawa na asilimia 67.75.
Kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa kufanya mtihani ni asilimia 96.38 walifanya mtihani na watahiniwa 279 sawa na asilimia 0.65 hawakufanya mtihani.
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kwa Naibu Katibu Mkuu Mtendaji (NECTA) Dkt. Charles Msonde. amesema ubora wa kufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha 35,880 sawa na asilimia 83.74 wamefaulu katika madaraja I-III wakiwemo wasichana 12,108 sawa na asilimia 87.30 na wavulana 23,772 sawa na asilimia 82.04.
EmoticonEmoticon