MABINTI WATOANA MANUNDU WAKIGOMBEA MWANAUME DAR ES SALAAM. STORI NZIMA HII


 
WAREMBO wawili, wakazi wa Sinza, Dar es Salaam ambao majina yao hayakupatikana, wamenaswa wakizichapa laivu wakidaiwa kugombea mwanaume.
Tukio hilo la kujidhalilisha lilijiri katika baa maarufu ya Corner iliyopo Sinza-Afrikasana, Dar, majira ya asubuhi wakati watu wakiwa kwenye mishemishe za kuwahi kazini.
 
Katika tukio hilo, mmoja wa warembo hao alikuwa akilalamika kuwa kuna mwanaume walikubaliana kwenda kuvunja amri ya sita fastafasta ili awahi kazini lakini akazidiwa ujanja na shosti wake hivyo akataka kukomboa chake na ndipo alipotolewa manundu.
 
Habari kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa warembo hao walijikuta wakizichapa kavukavu wakimgombea mwanaume huyo aliyedaiwa kuwa ni mume wa mtu, mwenye ndoa changa. 

Katika timbwili hilo lililojaza kadamnasi, wanaume walishuhudia sinema ya bure baada ya mmoja wa warembo hao kula kipigo kizito na kuvuliwa nguo ambapo alibaki wazi sehemu za makalio.
Previous
Next Post »