NAIBU SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AVIPONDA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI VINAVYO WASIFIA BAADHI YA WABUNGE WA VYAMA VYA UPINZANI WASIO NA NIDHAMU.

ndugai

Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai (pichani) amewataka wabunge kuwa na staha na kuacha utovu wa nidhamu pindi wanapojadili masuala yanayoihusu jamii ya watanzania kwa ujumla.

Amesema kuna baadhi ya wabunge wa vyama Fulani Fulani ambao hata wakifanya mambo ya ajabu vyombo vya habari vinafanya waonekane mashujaa na kuwa wako sahihi.

Aidha ameweka wazi kuwa pamoja na baadhi ya wabunge kuchana nyaraka halali za bunge lakini hakuna hatua zitakazochukuliwa labda kama kutajitoza utovu mwingine wa nidhamu kwa sababu kama ilivyo kiongozi unapochukua hatua ndio unaonekana mbaya.

Previous
Next Post »