Joseph Kony amekuwa akisakwa kwa muda mrefu
Marekani imeahidi zawadi ya dola milioni tano kwa yeyote
atakayetoa maelezo yatakayosaidia kukamatwa kwa kiongozi wa waasi wa Lords
resistance Army nchini Uganda Joseph Kony.
Bwana Kony anadaiwa kuongoza maasi ya zaidi ya miongo miwili nchini Uganda na
anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC kwa mashtaka ya uhalifu wa
kivita.
Tangazo hili limekuja huku jeshi la Uganda likiakhirisha msako wa kiongoiz
huyo wa waasi, katika jamuhuri ya Afrika ya kati, baada ya kusema kuwa
wanatatizwa na serikali mpya ya mpito.
Kony na wapiganaji wake wako katika maficho yanayopakana na nchi jirani za
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ikiwemo Sudan, Jamuhuri ya kidemokrais ya Congo na
Uganda.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa zawadi hiyo pia inatolewa kwa yeyote
atakayetoa taarifa kuwahusu viongozi wengine wa waasi wa LRA Okot Odhiambo na
Dominic Ongwen.
Kundi la LRA limewatesa watu na kuwadhalilisha watoto nchini Uganda, na kote
katika eneo hilo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alinukuliwa
akisema kwenye jarida la Huffington Post siku ya Jumatano.
Bwana Kerry alisema kuwa Kony na viongozi wengine wa LRA , hawatapatikana kwa
urahisi.
Kundi la LRA limetawanyika kwa makundi na waasi, walioko katika sehemu kubwa
ya nchi kwenye maficho ambayo kwa kweli ni vigumu kuyapata, wakitawala eneo hilo
kwa kutumia vitisho na kuwatia watu hofu.
Mapema, jeshi la Uganda katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, lilisitisha msako
wao wa Kony na kurejea katika kambi zao za kijeshi.
EmoticonEmoticon