Rais Zuma amesema wanajeshi wake wataondoka Afrika Kusini baada
ya serikali kupinduliwa
Afrika Kusini, inasema kuwa itawaondoa wanajeshi wake kutoka
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, baada ya waasi kupindua serikali zaidi ya wiki moja
iliyopita.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa mkataba kati ya nchi hizo mbili umetupiliwa
mbali baada ya kung'olewa kwa rais Francois Bozize.
Bwana Zuma anakabiliwa na hasira za wananchi baada ya wanajeshi 13 wa nchi
hiyo kuuawa katika mapinduzi ya kijeshi .
Alitoa tamko hilo katika mkutano wa dharura kuhusu mgogoro wa kisiasa katika
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambao marais wa nchi za magharibi walikataa
kumtambua kiongozi wa waasi kama rais wa taifa hilo.
Michel Djotodia alitangaza kuwa ataitawala nchi hiyo kwa kipindi cha mpito,
baada ya kundi la waasi wa
Seleka kuvamia mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui, na
kumaliza uongozi wa aliyekuwa rais Bozize, aliyetawala kwa mwongo mmoja.
Kiongozi huyo wa waasi amesema ataongoza nchi hiyo hadi uchaguzi
utakapofanyika mwaka 2016.
''Haiwezekani kwetu kumtambua mtu aliyejitangaza kama rais,'' alisema rais wa
Chad, Idriss Deby wakati wa mkutano huo.
Wanajeshi waliouawa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati wakati wa
haratakati za mapinduzi
Alisema Zuma aliwaambia viongozi hao kuwa anapanga kuondoa majeshi yake
nchini humo.
Afrika Kusini ilikuwa na takriban wanajeshi, 200 mjini Bangui, ambao kazi yao
ilikuwa kujaribu kuzuia waasi wa Seleka kumng'oa mamlakani bwana Bozize ambaye
kwa sasa yuko nchini Cameroon.
Pamoja na wanajeshi 13 kuuawa, wengine 27 walijeruhiwa, ikiwa idadi kubwa ya
wanajeshi kuwahi kuuawa nje ya nchi hiyo tangu kumalizika kwa enzi ya ubaguzi wa
rangi mwaka 1994.
Vifo hivyo vimesababisha tetesi nchini Afrika Kusini huku wakosoaji wakisema
kuwa wanajeshi walipelekwa nchini humo ili kulinda maslahi ya kibiashara ya
chama tawala.
Chama hicho hata hivyo kimekanusha madai hayo na kusema kuwa wanajeshi hao
walikuwa wanatoa mafunzo kwa wanajeshi wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati pamoja na
kulinda usalama.
EmoticonEmoticon