Akichangia Bungeni jana jumatatu-15/04/2013 jioni,Mbunge wa Iringa mjini,Mchungaji Msigwa,amewalaumu viongozi wa serikali ya CCM kwa kupuuzia mambo nyeti kama matatizo ya udini Zanzibar.
Msigwa alimlaumu vikali waziri Mkuu kwa kutoa jibu jepesi kwa swali alilouliza juu ya udini Zanzibar.Alisisitiza kwamba,kuwa na cheo kikubwa serikalini au kusoma hakumfanyi mtu mpumbavu awe mwelevu.
Akinukuu vifunguu kadhaa vya Biblia,Msigwa amesisitiza kuwa,"hata ukiutwanga upumbavu na mbegu kwenye kinu,upumbavu utabakia upumbavu".
Amedai kitendo cha viongozi wenye akili ndogo kuongoza watu wenye akili kuwazidi ndiko kulikopelekea mauaji ya kidini Zanzibar na migogoro mingine ya kidini ikiwepo tukio la mtu mmoja kukamatwa na bunduki ya kivita yenye risasi ndani ya kanisa la Anglikani jana.
Hoja hiyo iliamsha hasira za wabunge wa Zanzibar ambao licha ya kumtukana na kumwita Msigwa kuwa ni mchungaji wa nguruwe,walisisitiza kuwa serikali ya Zanzibar inaenzi dini ya kiislam na haiwezi kuruhusu uhuru wa mavazi kwa wanawake.
Huku akishangiliwa kwa nguvu na wabunge wa CCM na wale wa CUF, Mbunge mmoja toka Zanzibar alisisitiza :"wanawake wanaopenda kutembea uchi,waende Iringa,sio Zanzibar,Zanzibar inaongozwa kwa misingi ya dini ya kiislamu".
Baada ya kuruhusiwa na naibu spika,kuwasilisha MWONGOZO WA SPIKA,Msigwa aliwalaumu wazanzibari kwa kutokukubali ukweli kuwa SERIKALI HAINA DINI.
"Mnajidanganya,nchi hii haitakuja ongozwa na sheria za kidini,maana serikali haina dini" alisisitiza Msigwa
EmoticonEmoticon