ofisa
wa Upelelezi Mbozi akionyesha sehemu ya Mbolea mbovu ambayo imefumbiwa macho na
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania na kuitakatisha kama haina matatizo wala
madhara kwa wakulima
Katika
hali inayoonyesha kuna mchezo mchafu wa kuendelea kuwamaliza wakulima wilayani
Mbozi, shehena ya Mbolea mbovu iliyozuiwa kuuzwa mwaka jana hatimaye “upepo
umepita” na kuruhusu iendelee kuuzwa kwamba ipo juu
kiviwango!
Katika
hali hiyo wakulima wamekuja juu jana wakati wakishuhudia ufunguzi wa duka la
STACCO ambalo miezi kadhaa lilishuhudiwa likiwa limepigwa makufuli na kwa
mbwembwe nyingi ikiwemo msururu wa vyombo vya habari, lakini kwa jana ilikuwa
kimya kimya kufuli la kwanza likafunguliwa, likafuata la pili na hatimaye la
tatu!
Wakati
wananchi kwa macho yao meupe wakishuhudia mifuko iliyoganda ya Mbolea za UREA,
DAP, CAN na SA taarifa iliyotolewa kuruhusu kufunguliwa kwa duka hilo inatoa
maelezo kuwa ni Mbolea ya SA peke yake ndiyo iliyobainika kuwa na ubora hafifu!
ambayo ni mifuko 11 tu.
Hata
hivyo afisa anayesimamia ubora wa Mbolea katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi
Bi Shonyela amesema licha ya maelekezo kutoka juu mengine hayatatekelezeka kwani
kufanya hivyo itakuwa ni kuwamaliza wakuliwa wa wilaya yake kwakuzingatia kuwa
Mbolea iliyoganda kuto kufaa tena mashambani.
“nimeandikiwa
Mbolea aina ya SA pekee ndiyo isafirishwe chini ya usimamizi wa polisi kwenda
Dar es Salaam lakini ni mifuko 11tu! Wakati kuna mbolea aina nyingine ambazo ni
zaidi ya mifuko 50 hazina viwango vya ubora na taarifa imekuwa kimya”
alifafanua
Uchunguzi
wa haraka kwenye duka hilo unaonyesha kuwa mifuko16 ya DAP ilikuwa imeganda
wakati wa kufunga duka hilo mwezi September mwaka jana, UREA mifuko 16, CAN 11
na SA 11.
Ingawa
katika maelezo ya mkurugenzi wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA
ilionyesha kuwa wangeshirikiana bega kwa bega na TBS katika kuhakikisha viwango
vya bidhaa hiyo vinasimamiwa, maamuzi ya kuruhusu uuzwaji wa mbolea aina ya DAP,
CAN na UREA iliyoharibika kwenye ghala la STACO wilayani Mbozi yanajenga mawimbi
na mashaka kwa wananchi kuwa mamlaka imelainishwa na ama wamefumbishwa
macho!
Tanzania
hutegemea maabara yake ya Mbolea iliyopo Mlingano mkoani Tanga kuthibitisha
ubora wa bidhaa hizo hata hivyo kumekuwepo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya
maofisa wa serikali na kuwasaliti wakulima kutokana na makampuni yanayofanya
shughuli za usambazaji wa pembejeo na hasa Mbolea kushika keki kubwa katika
mzunguko wa fedha nchini
Wakati
pia chuo cha kilimo SUA kimekuwa kikitumika katika tafiti na uchunguzi wa
Mbolea, mwaka jana Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika Dr Adam Malima alikataa
matokeo ya uchunguzi wa mbolea yaliyotolewa na SUA na kuahidi sampuli za Mbolea
iliyokamatwa RUVUMA kupelekwa nchini Afrika kusini kujiridhisha na uchuguzi wa
maabara za huko baada ya kulalamikiwa na wakulima
Aidha
naibu waziri alisitisha leseni za makampuni ya STACO na Mohamed Enterpries mnamo
August 07 mwaka jana, ambapo baada ya siku kadhaa Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Udhibiti Mbolea Tanzania Suzana Ikelya alitua Mbozi na kukamata Mbolea kwenye
duka la STACO
“Maamuzi
ya mamlaka ya ukaguzi wa ubora wa Mbolea yanawaacha wananchi wilayani Mbozi
wakikosa imani kutokana na namna maamuzi yanavyofikiwa hata katika mambo ambayo
hayahitaji utaalamu kuthibitisha ubora kama suala la Mbolea iliyoganda” anaeleza
bwana Keneth Mwazembe mmoja wa wakulima wakubwa wilayani
Mbozi.
Msimamizi
wa duka la STACO bwana Julius Masai licha ya kufurahia kufunguliwa kwa ofisi
yake ya chakula, amesema ni kweli kwamba kuna mbolea ambayo haimo kwenye barua
ya kuruhusu uuzwaji ambayo haifai kwa matumizi lakini wanatumia busara kuitenga
licha ya kutoelezwa kwenye barua hiyo
Ni
kweli kuna mifuko kama 37 hivi ya mbolea mchanganyiko ambayo ni mbovu na
tumeitenga pembeni na hatutaiuza” alisema meneja huyo bwana Julius
Masai
Duka
hilo limefunguliwa jana chini ya usimamizi wa maofisa wawili wa idara ya
upelelezi ya jeshi la polisi na ofisa anayesimamia ubora wa MBOLEA wilaya ya
Mbozi, na shughuli hiyo imefanyika kimya kimya tofauti na mbwembwe zilizofanyika
wakati wa kufunga duka hilo ambapo wananchi waliokuwa wakipita barabarani
waliitwa kushuhudia namna wanavyotendwa!
Kwahisani
ya Indaba Africa
|
EmoticonEmoticon