Wanafunzi wa Sekondari ya Usevya Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi wamezishambulia familia mbili kwa kutumia silaha za jadi na kuwavunjia nyumba zao baada ya kuzituhumu familia hizo kuwa zinajihusisha na vitendo vya kishirikina uliopelekea kifo cha mwalimu wao
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hili lilitokea hapo juzi majira ya saa 12 alfajiri baada ya wanafunzi wa shule hiyo walipo pata taarifa ya kifo cha mwalimu wao Tumsifu Philimon (28) aliye fariki dunia katika Hospital ya Sumbawanga aliko kuwa akipatiwa matibabu usiku wa tukio hilo.
Kidavashari aliwataja walio vamiwa nyumba zao na wanafunzi kuwa ni Philipo Mwanjisi na Aprotina Mkalala ambapo mbali ya nyumba zao kuvunjwa walishambuliwa pia kwa kupigwa na mawe
Kabla ya tukio hili mmoja wa familia hizo alifika shuleni hapo wiki iliyo pita kwa lengo la kuonana na Mwalimu Tumsifu baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mtoto wake aliye kuwa akisoma hapo alikwenda mshitaki mwalimu huyo kwa mzazi wake kuwa amepingwa viboko na mwalimu Tumsifu adhabu ambayo mzazi huyo hakuridhika nayo
Inadaiwa baada ya mzazi huyo kufika shuleni hapo alimpa vitisho mwalimu huyo huku baadhi ya wanafunzi wakisikiza vitisho vilivyo tolewa na mzazi huyo wa mwanafunzi
Siku iliyo fuata mwalimu huyo aliamka akiwa anaumwa na ndipo alipo amua kusafiri hadi Sumbawanga waliko wazazi wake kwa lengo la kwenda kupata matibabu
Ilipofikia April 12 mwalimu huyo alitoweka hospital hadi hapo april 15 ambapo mwili wake uliokotwa akiwa amekufa kando kando ya mto huku akiwa amenyofolewa macho
Kamanda Kidavashari alisema wanafunzi hao walihisi kuwa kifo cha mwalimu wao kimesababishwa na kurogwa na wanakijiji hao wawili nandipo walipo amua kwenda kushambulia wanakijiji hao na kuvamia nyumba zao
Alisema upelelezi wa tukio hili unaendelea ili kuwabaini wanafunzi wote walio husika na tikio hilo na watakao bainika waweze kuchukuliwa hatua
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Gemela Rubinga alisema anategemea leo kwenda shuleni hapo ili kuzungumza na wanafunzi hao wa shule ya Sekondari ya Usevya ili kubaini chanzo cha vurugu hizo
Na Walter Mguluchuma
Katavi
EmoticonEmoticon