Cover la filamu hiyo ya
Sister Marry.
HATIMA ya filamu ya
mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa
kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji huyo amesalimu amri ya
viongozi wa kanisa hilo.Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama
Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa
ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi
mafupi.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu
hiyo.
Akipiga stori na paparazi
wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu
hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo
atakujairudia upya wakati mwingine. “Asilimia 85 ya filamu
niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa
nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo
baadaye,” alisema
Ray.
EmoticonEmoticon