MAMLAKA
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi nchini kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na Mamlaka hiyo katika kutekeleza hatua za uhamaji wa urushaji wa
matangazo kutoka Analojia kwenda Digitali.
Mwito
huo ulitolewa na Afisa Uhusiano wa Tcra Innocent Mungi wakati akizungumza na
Vyombo vya Habari vya Mkoa wa Mbeya katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa
mikutano wa Mkapa, kuhusu zoezi la uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Mkoa wa
Mbeya.
Mungi
alisema zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa Televisheni ya mfumo wa
Anaolojia ulianza kutekelezwa Disemba 31, Mwaka jana katika Jiji la Dar Es
Salaam kutokana na makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Alisema
wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwao kutokana maandalizi ya kuzima mitambo
hiyo katika Jiji la Mbeya kukamilika kwa kuwashirikisha wananchi wa Vitongoji
vyote ambapo mitambo hiyo itazimwa rasmi Saa sita Usiku Aprili 30, Mwaka
huu.
Afisa
huyo alisema Elimu kwa umma kupitia mbinu mbalimbali kuhusu mchakato wa kuhamia
katika Teknolojia ya mfumo wa Utangazaji wa Digitali imekuwa ikitolewa kwa
kiwango cha kuridhisha.
Alisema
matangazo ya Digitali ni mazuri kwa sababu huwafikia watazamaji wengi zaidi
kuliko Mfumo wa Analijia ambapo kati ya Watazamaji wanaofikia asilimia 24 ni
Asilimia 22 wanaofikiwa na matangazo hayo.
Kwa
upande wake Mhandisi wa Maswala ya utangazaji kutoka Mamlaka ya mawasiliano,
Andrew Kisaka alisema katika Awamu ya kwanza ya uzimaji wa mitambo hiyo itaishia
katika Mkoa wa Mbeya.
Alisema
hatua ya awamu ya pili itatangazwa baadaye ambapo aliitaja mikoa ambayo imezimwa
katika awamu ya kwanza kuwa ni Dar Es Salaa (31/12/2012), Dodoma na
Tanga(31/1/2013), Mwanza(28/2/2013), Moshi na Arusha (31/3/2013) na Mbeya
ambayo itazimwa mwishoni mwa mwezi huu.
Aliongeza
kuwa baadhi ya vigezi ambavyo viliwekwa na Serikali kabla ya kuanza kutekeleza
suala hilo ni pamoja na Kuhakikisha kuwa eneo linalozimwa lina huduma ya
matangazo ya Digitali, Elimu kwa umma itolewe kuhusu zoezi la uzimaji kabla ya
utekelezaji.
Alivitaja
vigezo vingine kuwa ni Kuendelea kuonekana kwa Chaneli tano za Bure ambazo ni
Tbc, Star Tv, Itv, Eatv na Capital Televisheni, Uwepo wa Ving’amuzi vya kutosha
katika eneo husika pamoja na kupunguza makali ya bei.
|
EmoticonEmoticon