Karim Wade
Mwanawe rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade, ametiwa
nguvuni kwa kujipatia dola bilioni 1.4 wakati wa utawala wa baba yake .
Karim Wade ambaye alihudumu katika serikali ya baba yake alikuwa na nyadhifa
mbali mbali wakati huo .
Wade aliwasilisha waraka wa orodha ya mali zake katika mahakama maalum ya
senegali iliyopewa jukumu la kuchunguza kesi za ufisadi jana asubuhi.
Alipewa muda wa mwezi mmoja kuthibitisha kuwa alichukua zaidi ya dola dola
bilioni kihalali wakati baba yake alipokuwa madarakani.
Karim Wade alipewa jina la bandia waziri wa anga na dunia , alipokuwa waziri
wa miundo mbinu , mipango ya miji , usafiri wa anga na ushirikiano wa kimataifa
kwa wakati mmoja.
Wakati huo pia alikuwa mkuu wa theluthi moja ya matumizi ya taifa . Mahakama
ya Senegali bado haijaeleza sababu ya kumtia rumande na mawakili wa Karim Wade
wamesema alichukuliwa kwa nguvu
EmoticonEmoticon