Aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak, amerejeshwa jela kutoka
hospitalini mjini Cairo.
Shirika la habari la nchini humo MENA limesema kuwa bwana Mubarak alipelekwa hospitalini viungani mwa mji wa Cairo akiwa chini ya uilinzi mkali.
Kiongozi wa mashtaka nchini humo aliamuru Mubarak kurejeshwa jela baada ya kuonekana mwenye nguvu huku akiwapungia mkono wafuasi wake.
Kesi ya mauaji ya waandamanaji dhidi yake itaanzishwa upya mnamo Jumatatu.
Maperma wiki hii mahakama iliamuru Mubarak kutolewa jela baada ya ombi la wakili wake kuwa miaka miwili imepita kabla ya kesi dhidi ya Mubarak kutofanyiwa uamuzi wowote katika kipindi hicho.
Chini ya sheria za Misri mtu hawezi kuwa jela zaidi ya miaka mahakama ikiwa haijatoa uamuzi katika kesi inayomkabili
EmoticonEmoticon