HISTORIA YA JOMO KENYATTA RAIS WA KWANZA WA KENYA AMBAYE NI BABA WA RIS WA SASA KENYA

Picha:Jomo Kenyatta.jpg

Jomo Kenyatta (1893-1978) alikuwa rais wa kwanza wa Kenya, alizaliwa mwaka 1893 jina lake halisi ni Johnstone Kamau wa Ngengi. Alipewa jina la utani ambalo ni Mkuki wa Moto (Burning Spear). Jina la Kenyatta lilitokana na mkanda aliopenda kuuvaa ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wagĩkũyũ wanauita kenyaata. Kabila lake lilikuwa ni Mgĩkũyũ. Alisoma katika shule ya kanisa la wamisheni wa Kiskoti.
Baada ya kuhitimu aliajiriwa kama karani na msoma mita wa manispaa ya Nairobi, alioa mke wake wa kwanza ambaye ni Grace Wahu.
Azma yake ya kutaka kuikomboa ardhi ya Wagĩkũyũ ilimfanya kuweza kuwaunganisha Wagĩkũyũ naye akawa katibu wao mwaka 1928.Katika mwaka 1930 alizuru Marekani na Uingereza ambako aliishi miaka kumi na mitano na hata kuoa mwalimu wa Kiingereza ambaye aliitwa Edna Kenyatta. Alirudi Kenya mwaka 1946 na alichaguliwa kuwa rais wa chama cha siasa cha Kenya African Union (KANU). Alihamasisha kukomeshwa ubaguzi wa rangi; kuwa na mwamko kisiasa pamoja na mambo mengine yanayompa Mwafrika heshima na utu. Aliandika kitabu kiitwacho Facing Mount Kenya kilichohusu ukombozi na historia ya Wagĩkũyũ. Alikuwa pia ni muhariri na muanzilishi wa gazeti la kwanza kwa lugha ya Gĩkũyũ ambalo liliitwa Mũigũithania.
Kutokana na kuhusishwa na harakati za vita vya msituni vya kundi la Mau Mau alihukumiwa miaka saba jela mwaka 1952. Huwezi kuzungumza historia ya Kenyatta bila ya kuitaja Maumau. Baadaye alioa mke mwengine wa tatu ambaye aliitwa Mama Ngina Kenyatta ambaye alikuja kuwa mke wa rais wa kwanza ambaye ndiye mama yake Uhuru Kenyatta. 1 Juni 1963 Kenya ilipata madaraka na Jomo Kenyatta alitawazwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kenya.
Kenyatta alifariki mjini Mombasa tarehe 18 Agosti 1978 na kuzikwa jijini Nairobi kwenye jengo la bunge.

Muda wa Utawala
12 Desemba 1964 – 22 Agosti 1978
Makamu wa RaisJaramogi Oginga Odinga
Joseph Murumbi
Daniel arap Moi
mtanguliziOffice created
aliyemfuataDaniel arap Moi

Muda wa Utawala
1 Juni 1963 – 12 Desemba 1964
MonarchElizabeth II
Governor GeneralMalcolm MacDonald
mtanguliziOffice created
aliyemfuataRaila Odinga (2008 – present)

tarehe ya kuzaliwa1894[1]Ichaweri, Gatundu, British East Africa
tarehe ya kufa22 Agosti 1978 (umri 83)Mombasa, Kenya
chama
ndoaGrace Wahu (m. 1919), Edna Clarke (1942-1946), Grace Wanjiku, Mama Ngina ( 1951-1978)
Previous
Next Post »