HAPPY BIRTHDAY AFANDE SELE


Seleman Msindi au Afande Sele (amezaliwa tar. 24 Aprili 1976) ni msanii wa muziki wa hip hop na Bongo Flava kutoka Mkoani Morogoro, Tanzania. Amewahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards mnamo mwaka 2004 kutokana na nyimbo yake ya 'Mtazamo' ambayo aliimba na Solo Thang na Professor Jay.pia alishinda tuzo ya (mkali wa rymes) mwaka [2003] kutokana na nyimbo yake ya 'darubini kali' aliyosmshirikisha Dogo Ditto.Ni muasisi wa makundi ya 'Ghetto Boys' na 'Watu Pori' ,yaliozaliwa na kufia mjini Morogoro kwa kufuatana na alikuwa msanii wa kwanza kuujaza uwanja wa mpira wa miguu wa JAMUHURI mjini morogoro alipozindua albam yake ya kwanza ya 'MKUKI MOYONI'.Aliongoza kampeni ya maleria mwanzoni mwamiaka ya 2005 na 2007..Mwanzoni wa mwezi wa 11 mwaka 2012 alitangaza rasmi kufanya kazi kama kundi jipya la watu pori baada ya kufanya kazi na MC KOBA ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda kundi la watu pori miaka ya nyuma
Previous
Next Post »