
Muigizaji wa  filamu nchini Dotnata Rubagumya anadai kuwekewa sumu kwenye juice na mtu asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa ya kiafya.
 Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa  kwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku  wakimweleza huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa  uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa  vipimo zaidi.
Anasema tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi  alikuwa akitapika.
 “Nimezidiwa usiku wa kuamkia  Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini  kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takriban mwezi wa  nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu aliipitisha kwa njia ya juice,”  amesema Dotnata ambaye kwa sasa ameokoka.
 Akizungumzia sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:
 “Kila mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda  hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua  mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili  niyasimulie mema ya Mungu. Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako  kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”
NA BONGO CLAN BLOG
EmoticonEmoticon