MWIGIZAJI zao la Kundi la Mambo Hayo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa swali alilokuwa akijiuliza juu ya wasanii wadogo kuwa na fedha nyingi za ghafla limepata jibu, kumbe zinatokana na wasanii hao kujiuza kwa vigogo.
Akiongea na mwandishi wetu, Cathy alisema tukio la Jack wa Chuz kunaswa hivi karibuni akienda kuuzwa, linatoa picha mbaya kwa wasanii wa kike hivyo anawasihi wote wenye tabia hiyo waache mara moja.
“Pato la kazi yetu ya filamu tunalijua, wengi tulikuwa tunawaona wakimwaga fedha nyingi kwenye sherehe mbalimbali pasipo kujua wapi wanazipata fedha hizo. Wasanii wanatakiwa kubadilika ili tuheshimike,” alisema Cathy.
Jumatano ya Februari 20, mwaka huu, Jack wa Chuz aliripotiwa na Gazeti la Risasi Mchanganyiko kuwa alinaswa akijiuza kwenye hoteli moja iliyopo Ubungo, Dar.
EmoticonEmoticon