NIMEPOKEA MAOMBI YA KAZI ZAIDI YA 700 KWENYE KAMPINI YANGU MPAKA SASA"..WEMA SEPETU




Siku chache baada ya Wema Sepetu kufungua kampuni yake ya Endless Fame na kutangaza nafasi za kazi maombi ya watu wakiomba kazi yamekuwa mengi kupita kiasi wakati nafasi zilizo tangazwa ni chache nafasi hizo ni graphic designer,editor,cameraman na personal secreatry.

Mtandao huu baada ya kufanya mahojiano ya kina na mmiliki wa kampuni hiyo mwanadada Wema Sepetu ili kutaka kujua mpaka sasa ni barua ngapi za maombi ya kazi hizo kasha zipokea dada huyo hakusita alifunguka na kusema kuwa maombi ya kazi ni mengi kuliko nafasi zilizo tangazwa na kufanya zoezi hilo kuwa gumu.


Mmoja ya wahusika wakubwa wa Endless Fame Film [Petit Man] alisema kuwa watu wanaotaka kufanya kazi na Wema Sepetu hadi sasa idadi yao ni kubwa na kwamba maombi yanazidi kuongezeka kadri ya siku zinavyozidi kwenda.

Kila siku maombi yanaongezeka kupitia barua pepe [email] na barua za kawaida.

Hadi kufikia asubui ya leo barua pepe [email] zilizopokelewa ni 568 na barua za kawaida ni 133 ambazo jumla yake ni 701 mpaka sasa . Mchakato bado unaendelea na watu waendelee kutuma maombi kwasababu siku ya mwisho kufanya application bado haijafika.


Previous
Next Post »