Makardinali washindwa kumpata Papa siku ya kwanza

 

Moshi mweusi ukiashiria hakuna papa mpya aliyechaguliwa siku ya kwanza baada ya makardinali kujifungia katika hekalu maalum, huko Vatican City
Makardinali katika ibada katika kanisa la St. Peter Basillica kabla ya kujifungia kumchagua Papa hapo jana
Siku ya kwanza ya uchaguzi wa papa mpya imeanza na hakuna dalili ya papa aliyechaguliwa baada ya moshi mweusi kuonekana angani kwenye bomba la moshi.

Zoezi la kumchagua papa atakayeongoza kanisa Katoliki duniani lilianza hapa jana Vatican City kwenye jumba maarufu la Sistine Chapel ambalo hutumika kwa ajili hiyo.
Makardinali wapatao 115 akiwepo Mudhama Policarp Kardinali Pengo wa Tanzania ni miongoni mwa walikusanyika kufanya zoezi hilo.
Yoyote kati ya makardinali hao anaweza kuwa papa mpya hivyo Kardinal Pengo naye ana nafasi ya kuwa papa mpya baada ya Papa Benedict xiv ambaye amestaafu.
Kwa sasa Papa Benedict amepewa jina jipya na ataitwa Papa Emaritus au Papa Emeritus wa Roma.
Kinachosubiriwa hapo kwa sasa ni moshi mweupe ambao ndio utakaonyesha papa mpya amepatikana na kama hajapatikana baada ya kupiga kura moshi mweusi utaonekana.
Makardinali hao watakaa katika jumba hilo hadi papa apatikane. Hawaruhusiwi kuwasiliana na mtu yoyote na watakuwa wakipiga kura mara nne kwa siku.


Mudhama Policap Kardinali Pengo (kulia) leo hii akiwa na Makardinali wenzake Vitican City
 
Mudhama Policap Kardiali Pengo kushoto akiwa na mmoja wa makardinali hapo jana mjini Vatican




Previous
Next Post »