LUKAS PODOLSKI amesisitiza kuwa anataka kubaki Arsenal na kurejesha nafasi yake ya kuwa chaguo la kwanza.
Podolski hajacheza kwa dakika zote 90 tangu Januari na mwezi ulipopita akahusishwa kuhamia Juventus au Atletico Madrid.
Mshambuliaji huyo wa Ujerumani ambaye alijiunga na Arsenal majira ya joto, alikiri kufurahishwa na kuhusishwa kwake na timu hizo.
Lakini nyota huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 10.9 jana akasema kuwa utashi wake ni kubakia Arsenal.
Alisema: Kwanza sina namna ya kuzisaidia timu hizo katika hilo la wao kunihitaji. Pili kunitaka kwako kunanifanya nijiskie fahari kwasababu inaonyesha kuwa nipo katika kiwango bora.
“Lakini sitegemei kuondoka hapa katika klabu na mji ambapo najiskia ni mwenye utulivu”.
EmoticonEmoticon