Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja
wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco.
Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali
za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka
huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika
hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka
Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff
(Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam),
Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir
Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe
(Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd
(Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi
Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana
Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kid
emokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon
Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars
linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa),
Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda
(Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
EmoticonEmoticon