RAY, JB, KING MAJUTO NA IRENE UWOYA WAITIKISA RWANDA

Vincent Kigosi, Irene Uwoya, Athuman Amri
 
Irene Uwoya
Irene Uwoya mwigizaji wa filamu Sawhiliwood
 

Jacob Stephen, Vincent Kigosi

JB akiteta jambo na Ray .


vincent Kigosi

Ray akifuatilia utoaji wa tuzo za Rwanda Movie Awards.


Vincent Kigosi, Irene Uwoya, Athuman Amri

King Majuto kwa nyuma na Ray , Irene Uwoya wakifuatilia kwa makini utoaji wa tuzo.


Irene Uwoya

Irene Uwoya akifuatilia Rwanda Movie Awards kwa makini.

WASANII nguli katika tasnia ya filamu Swahiliwood Ray, JB, King Majuto na Irene Uwoya walikuwa gumzo katika tamasha la utoaji tuzo nchi Rwanda ambapo msanii kama Irene Uwoya ilibidi jina lake la asili lipotee na kujikuta akikumbushwa enzi za nyuma alivyotesa katika filamu iliyotamba na kuwa gumzo ya Oprah on Sunday.
 
Matangazo katika redio televisheni jina lilokuwa likisikika ni Oprah
Wanyarwanda walilipuka ukumbi huku wakiita Oprah na Ray wakimwita Kigozi badala ya Kigosi, tuzo hizo zilizopewa jina la Rwanda Movie Awards zikilenga kuwatunuku wasanii wa filamu wa nchi hiyo na wasanii kutoka Bongo wakiwa kama watu mashuhuri waliofika kutoa zawadi kwa washindi walichaguliwa Rwanda Movie Awards.

Tamasha hilo la utoaji wa tuzo liliandaliwa na Ishusho Arts na kutoa mwariko kwa nyota wa filamu kutoka Swahiliwood, pia wasanii hawa waliweza kuona na viongozi wa nchi hiyo na kubadilishana mawazo kama wageni wanaowakilisha wasanii Afrika Mashariki.

 
Previous
Next Post »