MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka afunguka juu ya tatoo alizochora mchumba wake Mariki Bandawe, zinazoonyesha mchoro wa kopa . Alisema kupitia mchoro huo ni dhahiri kuwa mchumba wake amedhihirisha kuwa na mapenzi ya dhati
Rose alilazimika kufunguka juu ya hilo baada ya kupokea maswali mengi kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake kwenye mtandao wa kijamii 'Facebook' baada ya kuituma picha hiyo inayomuonyesha mchumba wake akiwa na mchoro kwenye bega lake la kushoto
Akizungumza Rose alisema kuwa mchoro wa mchumba wake ni dhahiri kuwa ana mapenzi ya dhati kwani ni wanaume wachache wanaweza kufanya kitendo alichokifanya yeye na kutuma picha kama hiyo ambayo inaonekana na watu wengi
"Unajua mpaka mtu inafikia hatua ya kuweka wazi ni kwamba unajiamini na chaguo lako na pia kwa upande wangu inaonyesha kunijali na kunilinda na baadhi ya magonjwa maambukizi kwa kutojihusisha na mwanamke mwingine," alisem Rose
Pamoja na hayo alizungumzia juu ya harusi yake ambayo amesema kuwa muda ukifika ataweka wazi tarehe na mwezi wa siku yao ya kufunga ndoa
Picha hiyo ilionekana kuleta utata baada ya mchumba wake kuituma picha kwenye mitandao ya kijamii 'facebook' huku baadhi ya mashabiki wakituma maoni yao juu ya picha hiyo na kutaka kufahamu nini maana ya alama iliyokuwepo kwenye picha.Chanzo:Pro24 blog
EmoticonEmoticon