Wabunifu mitindo Jackline Kibacha na Anna
Lukindo wakisindikizwa na Mama Balozi Joyce Kallanghe na Mama Rose
Kiondo.
Nje ya Jumba la
Somerset.
Wanamitindo wa Kitanzania kwenye London
Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline
Kibacha.
Mama Rose Kiondo, Samson Soboye, Mama Joyce
Kallaghe, Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline
Kibacha.
Anna Luks.
Anna, Jack na Duane kutoka
Jamaica
Barabara ya The Strand
copy.
London Fashion Week 2013.
(Picha zote za Urban
Pulse).
Imeandikwa na Urban Pulse na Freddy
Mach
Jumapili mchana wilaya ya Westminster jijini
London ilikuwa na mashindano ya ubunifu na urembo katika maonyesho ya kimataifa
ya London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset
lililosimama imara kwenye upembe wa kaskazi ya mto
Thames. Maonyesho ya London Fashion Week, bado
yanaendelea jumba hili la Somerset toka tarehe 14 hadi tarehe 28. Wiki hizi
mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na biashara ya mavazi na
urembo.
Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu,
walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na
wamiliki viwanda. Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji tu
vinavyojionyesha, bali pia watu wa
biashara.
Siku hii Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu
za Kiafrika zilizochaguliwa na British Council na LFW kushiriki kwenye
mashindano ya kutafuta vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na
urembo.
Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha na
Christine Mhando ndio wasanii waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha
katika mashindano haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka
27 sasa.
Katika kuunga mkono maendeleo ya Tanzania na
Watanzania, Ubalozi wetu Uingereza na Bodi ya Utalii Tanzania, nao pia
walichukua nafasi hii kuwasaidia wananchi hawa kufanikisha mahitaji yao ya
ushindani.
Ubalozi umetoa Ukumbi wa Nyumba Ya Tanzania
ulioko Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha nguo na sanaa zao kwa juma
zima kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru. Vile vile Bodi ya Utalii
ya Tanzania imesaidia katika mchango wa mali ghafi zilizotumika katika shughuli
hizi ili kuiuza Tanzania kimataifa.
Mshindi wa tukio alikua Estonia. Ingawa
Tanzania haikuwa mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora jambo ambalo
limetikisa nyoyo na vichwa vya waandaaji, wabunifu,wafanya biashara na watafuta
vipaji vya kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa letu kushiriki katika
shughuli na wote wameguswa na kupumbazwa na usanii wa hali ya juu ulioonyeshwa
na wasanii watatu wa Kitanzania.
Lukindo, Mhando na Kibacha wamechukua nafasi
waliyopewa kwa mikono miwili na wote wameisogeza Tanzania hatua moja zaidi ndani
ya ulingo wa kimataifa na katika biashara hii ya mavazi na urembo ambayo
inasemekana ina thamani ya Pauni Billioni 10 ama shilingi Trillion 25 za
Tanzania.
EmoticonEmoticon