Rapper na hitmaker wa ‘Nasema Nao’ Ney wa Mitego ameimbia‘exclusively’ Bongo5 kuwa hana mpango wa kumjibu Nikki Mbishi aliyeandika wimbo wa kumdiss uitwao ‘New wa Mitego’. Miongoni mwa mashairi kwenye wimbo huo yanasema, “’Ney wa mitego, anagawa ndogo ka gay mwenye pepo’.
Pia February 6, Nikki alitweet, ‘I am deeply in love with this shawty named @Nay wa mitego’.Bongo5 imeongea na Ney kuhusiana na issue hiyo ambaye amesema hana mpango wa kumjibu Nikki kwakuwa anatafuta pa kutokea.
“Anatafuta pa kutokea mimi sitaki kuongea lolote kuhusu yeye. Mimi sitaki kufuatilia kwasababu nimeshagundua kuwa ni upuuzi, yeye anatafuta njia ya kupita mimi sitaki kuzungumza chochote, hata interview yoyote kuhusu yeye sitaki, yaani nalizungumza hili kwasababu nyinyi ni wanangu (bongo5) lakini nimekataa, nimekataa kabisa, sitaki kabisa kumzungumzia huyo mtu,” amesema Ney.
“Kama kuna wananchi ambao ni matahira wanaweza kuelewa hicho alichokifanya it’s okay. Mimi huwa namuimba mtu kwa kitu ambacho kila mtu anakiona na ndio maana nimekuwa na mashabiki wengi sana kwasababu mimi huwa naongea ukweli. Nikisema Chidi Benz katoboa pua ni kweli
katoboa pua, sijawahi kumuimba mtu kwa matusi au nini kwahiyo siwezi kubishana na mtu wa aina hiyo. Kwanza hajulikani, hajui anafanya nini, kwanza yeye mwenyewe hajielewi, kujielewa hakuna mwanaume anasuka hata Ulaya kwenyewe waliacha, mtu wa design hiyo ni mtu ambaye hata nauli ya kwenda studio hana, ana matatizo.”
“Angekuja kuongea na mimi ningemwambia andika lyrics hizi ni poa zaidi hata wananchi watakuelewa.Siwezi kumjibu Nikki Mbishi hata siku moja. Yeye anahustle ili atoke kwenye muziki lakini mimi mwenzake naishi bila muziki so mimi naweza nikamlea yeye na akaishi vizuri, nikamtengenezea nywele zake anazosuka, nikamkodishia na salon kwenda kusuka kila anapohitaji. Sio mara ya kwanza, alishaniimba kabla ya hapa mimi nikachukulia poa,” alisisitiza Ney wa Mitego.
EmoticonEmoticon