MTOTO WA MWENYEKITI WA KIJIJI TANANGOZI IRINGA AJINYONGA KATIKA OFISI YA KIJIJI


 
 
Katika hali ya kusikitisha mtoto wa mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Tanangozi katika wilaya ya Iringa vijijini Doto Kikoti ameamua kujinyonga katika ofisi ya kijiji hicho inayoongozwa na babake mzazi kama njia ya kupinga kuwekwa kizuizini katika ofisi hiyo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo baada ya kijana huyo kutuhumiwa kufanya vurugu kubwa katika kijiji hicho na mzazi wake kuamua kumkamata na kumfungia katika ofisi hiyo ya kijiji kwa usalama wake.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kijana huyo alijinyonga kwa kutumia suluali yake akiwa ndani ya ofisi hiyo baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho ambae ni babake mzazi Bw Narbeti Kikoti kumfungia katika ofisi hiyo.

Mwili wa kijana huyo umetolewa eneo la ofisi hiyo majira ya saa 5 asubuhi leo na kupelekwa nyumbani kwa wazazi kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.


Previous
Next Post »