Kiasi watu 150 , ikiwa ni pamoja na watoto, wamejeruhiwa leo wakati treni zilipogongana karibu na mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria. Ajali hiyo ilitokea wakati treni ilipojigonga katika treni nyingine iliyokuwa imesimama karibu na Attridgeville, ambacho ni kitongoji cha mji wa Pretoria. Watu 20 wako katika hali mbaya , licha ya kuwa wengi wameondoka katika eneo hilo huku wakiwa na majeraha. Msemaji wa huduma za dharura Johan Pieterse amesema kuwa dereva wa treni moja kati ya hayo yuko katika hali mbaya.
Huduma za treni zimesitishwa kwa muda kutokana na ajali hiyo, ambapo sababu za ajali hiyo bado zinachunguzwa.
Afrika kusini ilitia saini mkataba wa dola bilioni 5.8 na kampuni ya Ufaransa ya Alston mwezi Desemba kuleta mabehewa mapya 3,600 ya treni kama sehemu ya mpango wa miaka kumi wa kufanyia matengenezo mfumo wa kizamani wa treni nchini humo.

EmoticonEmoticon