Israel yashambulia Lebanon

Urusi imesema leo kuwa ina wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za mashambulizi ya Israel dhidi ya Syria, ikionya kuwa mashambulizi kama hayo hayakubaliki na yanakiuka sheria za kimataifa. Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi imesema inachunguza madai kuwa ndege za kijeshi za Israel zimeshambulia kituo cha utafiti wa kijeshi cha Syria pamoja na ripoti nyingine kuwa msafara wa magari karibu na mpaka na Lebanon pia umeshambuliwa. Israel ilifanya mashambulizi hayo ya anga yasiyo ya kawaida ndani ya ardhi ya Syria, kwa mujibu wa maafisa wa Marekani , yakilenga msafara wa magari hayo yanayoaminika kuwa yalikuwa yamebeba silaha za kutungulia ndege zilizokuwa zinapelekwa kwa wanamgambo wa Hizbullah nchini Lebanon. Mtaalamu wa masuala ya haki za raia katika chuo kikuu cha mjini Jerusalem Alan Baker ni haki ya Israel kujilinda.
Mashambulizi hayo ni moja ya matukio hatari kabisa wakati huu, hasa ikitiliwa maanani hali ya wasi wasi iliyopo kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria. Taarifa iliyotolewa na jeshi la Syria kupitia televisheni ya taifa jana imesema kuwa ndege za kijeshi zilizokuwa zinaruka chini chini zilivuka mpaka na kuingia Syria katika eneo linalodhibitiwa na Israel la milima ya Golan na kushambulia kituo cha utafiti wa masuala ya kijeshi katika eneo la Jamraya, kaskazini magharibi ya mji wa Damascus.
Previous
Next Post »