Tetemeko la ardhi 6.8


Tetemeko la ardhi lililokuwa katika kiwango cha 6.8 katika kipimo cha Richter, limesababisha majengo kutikisika , kuharibu vifaa katika maduka na kuvunja madirisha ya majengo kaskazini mwa Chile. Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 55 katika mji wa Atacama amefariki kutokana na mshtuko wa moyo, amesema Meya wa mji huo Rafael Prohens, ambae amesema kifo cha mwanamke huyo kilitokana na hofu wakati wa tetemeko hilo. Maafisa wa Chile wamesema kuwa uharibifu ulikuwa si mkubwa sana na aliondoa uwezekano wa kuzuka kwa Tsunami. Tetemeko hilo lilitikisa mji mkuu Santiago, na kusababisha majengo kuyumba, lakini watu wamehisi zaidi tetemeko hilo katika eneo la kaskazini. Katika mwaka 2010, tetemeko kubwa lililokuwa katika kiwango cha 8.8 pamoja na Tsunami , liliuwa watu 551 na kuharibu nyumba karibu 220,000 pamoja na kuharibu kabisa eneo la bandari, majengo yaliyojengwa katika ukingo wa mto na bahari.
Previous
Next Post »