TAASISI mbili za kimataifa, zimeipatia Tanzania mkopo wa masharti nafuu wa jumla ya Sh36 bilioni, kwa ajili ya kugharimia mradi mkubwa wa maji katika Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, amezitaja taasisi hizo kuwa ni Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi kwa nchi za Afrika (Badea) na Umoja wa nchi zinazouzalisha Petroli kwa wingi Duniani (Opec).

Profesa Maghembe ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga, aliyasema hayo jana wakati akikabidhi vyeti kwa Bodi za Watumiaji Maji katika Wilaya ya Mwanga.
Alisema, Badea na Opec kupitia mfuko wake wa Opec Fund for International Development (Ofid), zimeipatia Tanzania Dola 22 milioni za Marekani sawa na Sh36 bilioni kwa ajili ya mradi huo.
Kwa mujibu wa Profesa Maghembe, fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi huo utakaovinufaisha vijiji 35 vya Wilaya za Same na Mwanga, mkoani Kilimanjaro na Korogwe, Tanga.
Kwa mujibu wa Profesa Maghembe, fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi huo utakaovinufaisha vijiji 35 vya Wilaya za Same na Mwanga, mkoani Kilimanjaro na Korogwe, Tanga.
“Hii ni ahadi ya Rais wetu Kikwete (Jakaya) kwamba anataka hadi kufikia mwaka 2015 tatizo la maji katika wilaya hizo tatu za tambarare liwe historia na tayari mtaaalamu mshauri yuko katika eneo la mradi,”alisema.
Profesa Maghembe alitumia fursa hiyo kuagiza kuanzishwa kwa Jumuiya za Watumia Maji katika maeneo yote ambayo hayana jumuiya hiyo na kuzitaka jumuiya hizo, kulinda vyanzo vya maji.
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Mwanga, Juma Yahya, alisema miradi mingi ya maji vijijini imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikwamo upungufu wa maji na uchakavu wa miundombinu.
Kwa mujibu wa mhandisi huyo, baadhi ya watumiaji wa maji bado wana dhana potofu ya “maji ya bure”.
Kwa mujibu wa mhandisi huyo, baadhi ya watumiaji wa maji bado wana dhana potofu ya “maji ya bure”.
EmoticonEmoticon