Idadi ya watu wasio na ajira imepungua mwezi Januari , na kufikisha idadi ya wasio na kazi kufikia kiwango cha asilimia 6.8 na kubakia karibu na wakati Ujerumani mbili zilipoungana. Takwimu za idara ya kazi nchini Ujerumani zinaonesha kuwa idadi ya watu ambao hawana ajira imepungua kwa watu 16,000 na kufikia sasa watu milioni 2.9, na kusitisha ongezeko la mara kwa mara la watu wasio na ajira. Taarifa hizo zitakuwa faraja kwa serikali ya nadharia za mrengo wa kati kulia ya kansela Angela Merkel, ambaye anakabiliwa na uchaguzi mwezi Septemba mwaka huu, uchaguzi ambao unaweza kuelekea katika kujadili suala la hali ya uchumi wa Ujerumani. Idadi ya watu wasio na kazi, ambayo ni suala muhimu sana nchini Ujerumani, ilifikia kwa mara ya kwanza katika kiwango cha watu milioni tatu tangu mwezi Machi mwaka jana , lakini idara ya kazi imesema masuala kadha yanayohusu misimu yamesababisha ongezeko hilo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon