Hillary Clinton atoka hospitalini

 
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Hillary Clinton ameondoka hospitali ya mjini New York ambako alikuwa anatibiwa maradhi ya mgando wa damu karibu na ubongo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema katika taarifa kwamba Waziri Clinton anaendelea vizuri na madaktari wanatarajia kuwa atapona kabisa. Clinton mwenye umri wa miaka 65 alilazwa hospitalini siku tatu zilizopita.

Mgando wa damu kwenye sikio lake la upande wa kulia unadhaniwa kuwa umetokana na kuumia kwenye ubongo baada ya kuanguka wiki mbili zilizopita.
Wasaidizi wake wamesema alizirai baada ya kupungukiwa maji mwilini kutokana na kirusi cha tumboni. Waziri Clinton anatarajiwa kujiuzulu kabla ya Rais Barack Obama kuanza rasmi muhula wake wa pili mnamo mwezi huu. Seneta John Kerry ameteuliwa kuchukua nafasi ya Clinton.
Previous
Next Post »