RaisJakaya Mrisho Kikwete
akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi
ya Kisutu jijini Dar es salaam
Jeneza lenye mwili
wa marehemu Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki ukiwasili kwenye makaburi ya
Kisutu,Upanga jijini Dar kwa ajili ya mazishi.
Baadhi ya watu
waliofika kwenye mazishi ya marehemu sajuki jioni ya leo Kisutu,jijini
dar.
Mbunge wa jimbo la
Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe akifafanua jambo mbele ya baadhi ya Wanahabari
kabla ya mazishi ya marehemu Sajuki,yaliyofanyika leo Kisutu jijini Dar es
salaam na kuhudhuriwa na maelfi ya watu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza jambo na Meya wa Wilaya ya Ilala,Mh Jerry
Silaa ,shoto ni Rais wa Shirikisho la wasanii wa
Filamu nchini,Simon Mwakifwamba akisikiliza .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
na baba mzazi wa marehemu Sajuki (pichani shoto) wakati wa mazishi ya msanii
huyo leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.Pichani kati Rais wa Shirikisho
la wasanii wa Filamu nchini,Simon Mwakifwamba na mwisho kabisa Meya ya Wilaya ya
Ilala,Mh Jerry Silaa.PICHA NA
IKULU
Mwandishi mkongwe wa
kampuni ya Uhuru Publications akiitafusta taswira murua kabisa kwenye mazishi
ya marehemu Sajuki,yaliyoongozwa na Rais Kikwete mapema leo jioni kwenye
makaburi ya Kisutu,Upanga jijini Dar.
Baadhi ndugu jamaa na
marafiki waliofika kwenye mazsishi ya marehemu Sajuki,wakisubiri mwili wake
waupokee kwa ajili ya maziko
EmoticonEmoticon