RC NJOMBE APIGA MARUFUKU WAKULIMA NJOMBE KULIMA KTK CHANZO CHA MAJI

 

 


Mkuu wa mkoa wa Njombe Aser Msangi (kulia) akiuagiza uongozi wa kata ya Mdandu kuzuia kilimo kwenye chanzo cha maji

RC Njombe akipanda mti leo


Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Astelina Kilasi akipanda mti


katibu tawala wa mkoa wa Njombe akipanda mti


MKUU wa mkoa wa Njombe kepteni ( mstaafu ) Aser Msangi aagiza wakulima wamaolima kando ya chanzo cha maji cha Nyolombo kata ya Mdandu wilaya ya Njombe kuondolewa mara moja.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo leo wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti katika mkoa huo wa Njombe uzinduzi uliofanyika katika Kijiji cha Mngeta Kata ya Mdandu katika wilaya ya Njombe kimkoa.

Msangi ambae kabla ya kuwahotubia wananchi katika uzinduzi huo alipata kushiriki zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji cha Nyolombo na Kutembelea maeneo mengine ya vyanzo vya maji ,alisema kuwa hajapendezwa hata kidogo kuona wananchi wakiendelea kulima katika chanzo cha maji huku viongozi wa Kijiji hadi wilaya wakiendelea kuwafumbia macho waharibifu hao wa chanzo cha maji.

Hivyo alisema kuwa ili chanzo hicho kiendelee kuwa endelevu ni vema viongozi wa ngazi ya Kijiji hadi wilaya kusimamia agizo lake hilo la kuwaondoa wavamizi hao wa chanzo cha maji.

Pia aliuagiza uongozi wa kata hiyo kuhakikisha wanarudia upya kazi ya kutengeneza barabara ya Kuzuia moto katika maeneo ambayo wamepanda miti ili kuepusha moto kichaa kuteketeza miti hiyo.

Kwa Upande wake mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Estelina Kilasi alimweleza mkuu huyo ya mkoa hatua ambazo wilaya hiyo imezichukua dhidi ya wamaolima katika chanzo cha maji cha Nyolombo kuwa ni pamoja na kuorodhesha majina yao na kukaa nao kikao na kuwaeleza kuwa baada ya kuvuna mazao yao mwaka huu kuto rudia tena kulima mashamba hayo ambayo yapo jirani na chanzo cha maji.

Nae afisa misitu mwandamizi Haji Mpya ambae pia ni kaimu meneja wa wakala wa misitu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini alisema kuwa mbali ya uhamasishaji mkubwa wa upandaji miti na utunzaji wa mazingira ambao ofisi yake imekuwa ikiufanya kwa Halmashauri za mikoa ya nyanda za juu kusini ila bado Halmashauri zimekuwa zikitoa takwimu za uongo juu ya miti iliyopandwa na iliyopo.

Mpya alisema kuwa ili kuwa na takwimu sahihi ofisi yake itaanzisha zoezi la ufuatiliaji wa takwimu za miti ili kuona toka zoezi hilo lilipoanzishwa kwa zaidi ya miaka 5 sasa ni miti mingapi iliyopo badala ya kuwa na takwimu za kwenye mafaili ila ukienda maeneo yaliyopandwa miti hiyo hakuna mti uliopona
Previous
Next Post »