Nilikamatwa kama mteja wa makahaba-mshtakiwa



Mahakama

MSHTAKIWA anayekabiliwa na shtaka la wizi na unyang’anyi wa kutumia silaha, Shida Rwanda, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa yeye hayafahamu mashtaka yanayomkabili kwa sababu alikamatwa kama mteja wa makahaba.Rwanda aliyasema hayo jana wakati akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo.
Rwanda alidai kuwa usiku wa Desemba 10, mwaka 2010 u akiwa katika kituo cha basi cha Studio, Kinondoni walitokea wasichana sita ambao walitaka kuvuka barabara.
Alidai kuwa yeye alikuwa akivuka kwenda upande wa pili lakini akiwa katikati ya barabara, walitokea vijana waliovalia nguo za kirai na kumweleza yeye pamoja na hao wasichana kuwa wako chini ya ulinzi.
Alidai kuwa baada ya kuwaweka chini ya ulinzi waliwaambia kuwa kwa wakati huo walikuwa wanaendesha doria kwa ajili ya kukamata makahaba na watu wanaoshirikiana nao.
“Mheshimwa askari hao, walinihusisha mimi kama mteja wa makahaba na baada ya muda yalitokea magari mawili ambayo moja lilikuwa na askari wanne wenye silaha na lingine likiwa na mtu mmoja ambaye kwa sasa ni RCO mkoani Arusha, Camillius Wambura na dereva,” alidai.
Alidai kwamba alimfahamu Wambura kwa sababu aliwahi kuwa na kesi katika Mahakama ya Kisutu, wakati huo na alikuwa akishikilia jalada lake.
Alendelea kudai kuwa baada ya Wambura kumwona, alimhoji kulikoni kuwepo uraiani wakati kwa mawazo yake aliamini yupo jela.
“Nilimjibu mahakama iliniachia baada ya kuniona sina hatia. Hakuniamini akatoa pingu nikafungwa na kupandishwa kwenye gari lililokuwa limebeba askari wanne na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay Desemba,” alidai Rwanda.
Mshtakiwa huyo alidai kuwa alipofika katika kituo hicho cha polisi, baadaye walimhamishia katika kituo kingine cha polisi cha Kijitonyama ambapo walianza kumtesa. Alidai kuwa kuanzia Desemba 11 hadi 19,2010 askari walikuwa wakibadilishana kwa ajili ya kumtesa na kwamba walikuwa wakimvua nguona kumwagia maji na kumpiga.
Aliendelea kudai kuwa Desemba 20, mwaka 2010 nyakati za usiku alifika askari wa nyota moja akiongozana na askari wengine wakamchukua hadi mapokezi ambako askari walimwambia kuwa hana thamani wala faida yoyote kwa sababu alimjibu bosi wao jeuri na kwamba watamnywesha simenti.
Baadaye yule askari wa nyota moja alitoa jalada moja kubwa na kuniambia nisaini, ilinilazimu kukubaliana naye kulingana na mateso na kipigo nilichokipata.
Hakimu Tarimo aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 7, mwaka huu kwa ajili yamshtakiw ahuyo kuhojiwa na upande wa mashtaka.
Katika kesi hiyo namba 256 ya 2010, Rwanda na wenzake Samwel Hezron, Hati Jawadu na Ismail Juma.
Previous
Next Post »