BAADA ya kutokea kwa hali ya vurugu nchini Misri rais wa nchi hiyo Mohammed Mursi ametanganza hali ya hatari katika miji ya Port Said, Suez na Ismalia.

BAADA ya kutokea kwa hali ya vurugu nchini Misri rais wa nchi hiyo Mohammed Mursi ametanganza hali ya hatari katika miji ya Port Said, Suez na Ismalia.
Kiongozi huyo aliyasema hayo alipokuwa akihutubia taifa ambapo alisema kuwa kuanzia jana hadi siku 30 zijazo watu hawataruhusiwa kutoka nje kuanzia muda wa saa 3:00 na 6:00.
Alisema aliamua kutoa wito huo kwa ajili ya kuwalinda wananchi wake kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo.
“ Kwa kawaida huwa napenda kuweka hali za tahadhari, na kutokana na vurugu zinazoendelea inabidi niwalinde wananchi kwa kukomesha umwagikaji damu basi,” alisema Mursi.
Hayo yalisemwa baada ya kutokea kwa mauaji ya watu takriban 33 waliofariki wiki iliyopita katika eneo la Port Said, ambapo uamuzi wa mahakama unadaiwa kuwa ulisababisha kuzuka kwa vurugu hizo pamoja na nyingine kutokea katika maeneo mengine ya nchi kutokana na kutoridhika na uongozi wa Mursi.
Hali hiyo iliendelea hadi katika mji mkuu wa Cairo, ambapo waandamanaji walikuwa wakipinga serikali na kupambana na vikosi vya ulinzi karibu Uwanja wa Tahrir kwa siku ya nne mfululizo.
Upande wa upinzani ulimlaumu Mursi kwa kutawala kimabavu na kuipa kipaumbele katiba mpya ambayo hailindi kikamilfu haki za kuabudu wala za maoni pamoja na kushindwa kudhibiti hali ya uchumi ambayo inazidi kuzorota nchini humo.
Hata hivyo licha ya kuwepo kwa pingamizi kutoka kwa upande wa upinzani Mursi alisema kwamba yupo tayari kuchukua hatua zaidi kwa ajili ya Misri na kwamba ilikuwa ni wajibu wake kama rais kufanya hivyo.
Katika harakati za kuhakikisha vurugu zinaisha nchini humo Morsi aliamua kuwaalika viongozi wa kisiasa wakutane kwa ajili ya majadiliano ya kitaifa.
Mbali na mwaliko wa viongozi hao pia muungano wa vyama tofauti nchini humo zaidi wa vyama pinzani nchini Misri, National Salvation Front, uliuunga mkono mwaliko huo, na kukubaliana na sera za Mursi.
Vurugu zilizuka eneo la Port Said baada ya mahakama kuwahukumu adhabu ya kifo watu 21 kwa kuhusika na fujo baada ya mechi ya kandanda Februari 2012.
Previous
Next Post »