Netanyahu meets with Merkel in Berlin

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Berlin. Viongozi hao wawili wamekutana jana usiku kwa chakula cha jioni kabla ya kile kinachoonekana kuwa ni siku ngumu ya mazungumzo. 

Israel imetangaza kuwa inaendelea na mipango yake ya kujenga makaazi mapya ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi. 

Mipango hiyo inaangaliwa na wengine kama hatua ya kulipiza kisasi uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuitambua Palestina kama taifa mwanachama asiye wa kudumu katika Umoja huo. Ujerumani iliikasirisha Israel kwa kususia kura hiyo. 

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujeruman Guido Westerwelle amekiri kwamba uhusiano umeharibika tangu Israel ilipoanzisha mipango hiyo mipya ya ujenzi wa makaazi, hatua ambayo imeshutumiwa kote ulimwenguni.

 Rais wa Palestina Mahmud Abbas ameutaja mradi huo, ambao huenda ukaugawanya Ukingo wa Magharibi na kufanya iwe vigumu kupatikana taifa la Palestina, kuwa ni wenye kuvuka "mstari mwekundu" jambo lisilokubalika.
Previous
Next Post »