*Mwananchi mmoja achomwa
mkuki,Polisi wakimbia.
Ugomvi baina ya Wafugaji wa
Wakulima umezuka katika Kijiji cha Simike - Utengule Usangu, Wilaya ya Mbarali
Mkoani Mbeya na kusababisha mwananchi mmoja anayefahamika kwa jina Abeli
Mwakyoma kujeruhiwa baada ya kuchomwa mkuki na kundi la wafugaji wa jamii ya
Kisukuma.
Wananchi watatu wanaofahamika kwa
jina la Bi. Magreth Simwela, John Kayange na Richard Mwasyanga walinusurika
kupigwa na kundi la wafugaji waliokuwa na kundi la ng'ombe, hali iliyopelekea
kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Igurusi.
Aidha Polisi wa kituo hicho
walifanikiwa kuwakamata Juma Mwambeta, Daniel Edward, Stephen, Walusungo Vaisi
na Vedasto Simwaba wakidaiwa kuwafungulia ng'ombe kutoka zizini na mara baada
ya kupata taarifa, Polisi walilazimika kwenda eneo la tukio na kukuta kundi
jingile la ng'ombe likila mazao shambani.
Baada ya ng'ombe kukusanywa mifugo
hiyo kundi la wafugaji lilianza kuwashambulia Askari na wakulima kwa kutumia
silaha za fimbo na mikuki, hali iliyopelekea Polisi hao kukimbia..
Kupitia
sakata hilo wafugaji walifanikiwa kumkamata Bwana Abeli Mwakyoma na kuanza
kumshambulia na alipofanikiwa kukimbia alichomwa mkuki kiunoni na baada ya
umbali kadhaa aliomba msaada wa kunasuliwa mkuki huo na kukimbizwa katika
Hispitali ya Chimala Mission,ambapo alilazwa na kuruhusiwa Oktoba 9 mwaka huu
baada ya kupatiwa huduma ya matibabu
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya. |
EmoticonEmoticon