WAISLAMU JIJINI DAR WACHARUKA KUFUATIA KUTIWA MBARONI KWA SHEIKH PONDA ISSA PONDA.




Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam Suleiman Kova akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda ambapo amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine Sheikh huyo anahusishwa na kundi lililovaamia kiwanja No. 311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe katika Manispaa ya Temeke mali ya Kampuni ya AGRITANZA.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.
 
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam Sulemain Kova amesema amesema jeshi hilo limechukua hatua hiyo kutokana na Sheikh huyo kutuhumiwa na makosa mbalimbali ya kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani.
 
Hata hivyo leo katika jiji la Dar es Salaam kumekuwa na patashika katika ya polisi wa kutuliza ghasia baina ya waandamanaji waliokuwa wakitaka Sheikh huyo kuachiwa pamoja waumini wengine wanashikiliwa.
Previous
Next Post »