TAARIFA KUTOKA KWA IGP MWEMA

Usiku wa kuamkia leo 13/ 10/ 2012 zimepatikana taarifa zilizothibitishwa juu ya mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow. IGP Said Mwema ametoa taarifa juu ya mauaji hayo.

Ifuatayo ni taarifa kamili kutoka kwa IGP Mwema:

"1.Ndugu wananchi. Napenda kuchkua nafasi hii kuwapa taarifa kuhusu mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa polisi Liberatus Barlow yaliyofanywa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia leo 13/10/2012 majira ya saa saba usiku Mkoani Mwanza.
...

2. Tukio hilo limetokea wakati kamanda huyo akitokea kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake eneo la Florida hotel Mwanza mjini, akiwa na ndugu yake waliyeongozana naye kutoka kwenye kikao hicho. Wakati akimshusha huyo ndugu yake eneo la Kitangiri minazi mitatu, walitokea watu wanaosadikika kuwa ni majambazi, na kumvamia na kuanza kumshambulia kwa risasi na kumuua hapo hapo.

3. Ndugu wananchi, kufuatia tukio hilo, tayari nimemtuma Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai DCI Robert Manumba kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha ulinzi na upelelezi wa tukio hilo.

4. Najua tukio hili limeshitua na kutuhuzunisha wote. Hivyo, wakati tukiendelea na taratibu zingine kuhusiana na tukio hilo, niwaombe wananchi wote kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi utakaowezesha kuwabaini wahalifu hao.

5. Tutaendelea kuwapa taarifa za tukio hilo, kadri tutakavyoendelea kuzipata."
Previous
Next Post »